Habari Mpya

Monday, 15 February 2016

Kizza Besigye azuiliwa na polisi Uganda

Mgombea urais wa chama cha upinzani cha FDC nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa na kuzuiliwa kwa muda na maafisa wa polisi mjini Kampala.
Gari lake lilikuwa likipitia barabara ya Jinja, mjini Kampala, msafara wake ukisindikizwa na mamia ya wafuasi, pale polisi walipotumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao na wakamkamata mwanasiasa huyo.
Dkt Kizza Besigye amegombea urais dhidi ya Museveni mara tatu awali

Alizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi cha Kira Road lakini akaachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka.
Polisi wanasema alikamatwa kwa sababu ya kutatiza uchukuzi mjini.

Bw Besigye alipangiwa kufanya mikutano ya kampeni katika mji huo mkuu.
Mkuu wa Polisi Jenerali Uganda Kalekezi Kayihura amethibitisha kwamba polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani lakini akakanusha habari kwamba Bw Besigye amekamatwa.
Maafisa wengine wa polisi walisema kiongozi huyo wa upinzani alizuiliwa tu kwa muda.

Hali ya wasiwasi ilitanda katika maeneo ya Kampala huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu. Watu kadha walikamatwa.
Bw Besigye, alikuwa wakati mmoja daktari wa kibinafsi wa Bw Museveni, amekamatwa na kuzuiliwa mara nyingi lakini Jumatatu ilikuwa mara ya kwanza kukamatwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika Alhamisi.
Bw Besigye amewania urais mara tatu dhidi ya Bw Museveni bila mafanikio.
Wafuasi kadha wa Besigye wamekamatwa na polisi
kwa hisani ya BBC


Next
This is the most recent post.
Older Post
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Kizza Besigye azuiliwa na polisi Uganda Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top