Habari Mpya

Wednesday, 6 January 2016

KIONGOZI WA UPINZANI AUWAWA BURUNDI

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi, Zedi Feruzi pamoja na mlinzi wake wamepigwa risasi jana Jumamosi na watu wasiojulikana katika mji mkuu Bujumbura. 

Akizungumza na chombo cha habari cha Reuters, Anshere Nikoyagize mkuu wa shirika la kiraia la Ligue ITEKA amesema Zedi Feruzi, kiongozi wa chama cha UPD na mlinzi wake walipigwa risasi katika wilaya ya Ngagara karibu na nyumbani kwake. 

Tukio hili limeongeza wasiwasi nchini humo baada ya mwezi mmoja wa maandamano yaliosababisha vurugu  kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu madarakani, hatua ambayo wapinzani kama Feruzi wanasema ni kinyume cha katiba.

 Hata hivyo rais Nkurunziza hajaonesha dalili yoyote ya kubatilisha uamuzi wake. Awali mahakama ya katiba ilitoa uamuzi kwamba rais Nkurunziza anapaswa kuwania kipindi kingine kwa sababu kipindi cha kwanza cha uongozi aliteuliwa na bunge na si kuchaguliwa na wananchi. Katiba ya Burundi inampa rais vipindi viwili tu vya uongozi.
Habari na dwswahili

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KIONGOZI WA UPINZANI AUWAWA BURUNDI Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top