Habari Mpya

Thursday, 7 January 2016

Je, Ni kweli mwandishi kavujisha mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or 2015, hili ndio jibu la FIFA …


Michael Abbink ni moja kati ya waandishi wa habari mahiri ila aliingia kwenye headlines hivi karibuni kutokana na tweet aliyoweka katika account yake ya twitter kuleta maswali. Ikiwa bado siku nne tuweze kushuhudia tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ikitolewa January 11 2016 Zurich Uswiss.

Abbink alipost tweet ambayo inaashiria kuwa Lionel Messi tayari ni mshindi wa tuzo hiyo. hivyo watu kuanza kuhoji ni kweli mshindi wa tuzo hiyo atakuwa ni Lionel Messi au mwandishi huyo wa kidachi kaandika kwa utashi wake na sio kwamba jina la mshindi wa tuzo hiyo limevuja.

Michael Abbink ni mwandishi wa NU Sport. Stori hiyo ya mwandishi Michael Abbink, shirikisho la soka ulimwenguni FIFA imebidi izikanushe na kuweka ukweli sawa kuwa bado mshindi hajulikana  na wala jina la mshindi halijavuja kama ilitangazwa awali.
aa


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Je, Ni kweli mwandishi kavujisha mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or 2015, hili ndio jibu la FIFA … Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top