.
Na Mwandishi Maalum, New York
Imeelezwa kuwa waandishi wa habari
pamoja na vyombo wanavyofanyia kazi wana nafasi kubwa ya ama kuchochea uibukaji wa
machafuko katika nchi zao au kuyazuia
kwa kutumia kalamu zao.
Hayo yameelezwa siku ya
Alhamis hapa Makao Makuu ya Umoja
wa Mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa
mfumo mpya wa uchambuzi unaolenga kutathmini viashiria hatarishi vya uhalifu, mauaji ya kimbari ,uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu
wa kivita
Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano
baina ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa
kuhusu Mauaji ya kimbari na Ofisi ya Umoja wa
Mataifa kuhusu wajibu wa kuwalinda raia (R2P) iliandaliwa kwa ushirikiano wa Wakilishi za Kudumu za
Tanzania na Italia katika Umoja
wa Mataifa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa mauaji ya Kimbari na
ulinzi wa Raia. Uzinduzi uliohudhuriwa
na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson.
Mfumo huo( framework of Analysis for Atrocity Crimes, a tool for
prevention) pamoja na mambo mengine licha ya
kutoa ufafanuzi, tafsri na
maelezo ya kina kuhusu viashiria na mazingira ambayo yanaweza kupelekea au
kusababisha mauaji ya halaiki au
kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa makosa ya kivita unapanua wigo wa kuvishirikisha vyombo vya
habari na asasi za kiraia kama wadau
muhimu wa si tu kufanya tathmini ya awari ya viashiria hivyo lakini ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za mapema za kuuzia kuibuka kwa
matatizo hayo katika jamii.
Vyombo vya habari na Asasi za kiraia
vinaelezwa kama wadau muhimu licha ya ukweli kwamba wajibu wa kwanza wa kuzuia
machafuko ya aina yoyote ile pamoja na
kutoa ulinzi wa raia ni wa
serikali kuu.
Na kwa sababu hiyo imeshauriwa kuwa waandishi
wa habari wanapashwa kwanza kutambua vyema viashiria hatarishi dhidi ya Amani na usalama
na kuwa nyenzo muhimu ya kuzuia kuibuka kwa
uhalifu huo badala ya kuwa sehemu
ya uhalifu huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson amesema ,
mwaka 2014 umeshuhudia umwagaji
mkubwa wa damu kuliko miaka mingine yoyote.
Amesema hali hiyo inatoka na ama kwa Jumuiya ya Kimataifa kutotambua
mapema na katika hatua za awali za
dalili ya kutokea uhalifu na uhalifu
dhidi ya binadamu au ni kwa jumuiya ya
kimataifa kutofautiana kimtazamo na kimaslahi kuhusu njia muafaka za
kuzuia uhalifu huo.
Akasema uzinduzi wa mfumo huo unatoa fursa kwa serikali na wadau wengine ya kutambua mapema viashiria vya uwepo wa
mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binafamu na uhalifu wa kivita.
Lakini kubwa na la msingi anasema ni
kuzuia uhalifu huo kabla
haujatokea.
Amesisisitiza kuwa uhalifu dhidi ya binadamu hauibuki mara moja, bali ni jambo linalokuwa
limepangwa na kuandaliwa kwa muda mrefu ukiwashirikisha wadau
mbalimbali.
Amesema hali ilivyo
hivi sasa ni kwamba jumuiya ya kimataifa imejikuta ikijikita zaidi katik a kushughulikia matatizo ambayo tayari
yameshajitokeza badala ya kuyazuia
katika hatua za awali hali
inayosabibisha kutumia gharama kubwa zaidi.
Kwa upande wake Naibu Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, pamoja na
kuelezea umuhimu na manufaa ya mfumo huo
wa tathmini ya viashiria
vya uwepo wa mazingira hatarishi. Amesema Tanzania inaunga
mkono ushirikishwaji wa wadau mbalimbali
kama sehemu muhimu katika eneo zima la Amani, usalama na ulinzi wa raia.
Hata hivyo ametahadharisha kuwa
pamoja na kutambua mchango wa wadau wengine, ni vema basi pawepo na utaratibu wa
uwajibikaji wa wadau hao ikiwa ni pamoja
usimamizi lengo likiwa ni
uwajibikani kama baadhi ya wadau
hao wanakuwa chanzo au chachu cha machafuko hayo.
Aidha
Balozi Mwinyi amesema Tanzania
ni rafiki wa mchakato huo
wa wajibu wa kuwalida raia (R2P).
Lakini ni ukweli usionpingika kuwa dhana hiyo ya
wajibu wa kuwalinda raia bado
imegubikwa na utatamwingi na kwamba kwa nchi nyingi hususani za afrika
bado dhana hiyo haijakubalika au haijapokelewa vema.
Amesema sababu ya kutopokelewa vema
kwa dhana hiyo na waafrika kunatokana na ukweli kuwa dhana hiyo inalenga zaidi
katika kuingilia masualaya ndani ya nchi
husika na pia ni dhana inayolenga katika kuleta mabadiliko ya kiuongozi
katika nchi husika ( regime change).
Na kwa sababu hiyo, Mwakilishi huyo
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa amesisitiza haja na umuhimu wa kuwapo na
usimamizi na utambuzi maalumu kuhusu dhana
hiyo ya wajibu wa kulinda raia bila
ya kuingilia uhuru wa nchi husika.
Katika uzinduzi huo, baadhi ya
wachangiaji wa mfumo huo wa thathmini pamoja na dhana ya R2P akiwamo Katibu Mkuu
Msaidizi Mwandamizi anayehusika na masuala ya
uzuiaji wa mauaji ya kimbari, Bw. Adama Dieng wameielezea Tanzania kama nchi ambayo ni
kielelezo halisi cha Amani, usalama na utulivu ikilinganishwa na mataifa mengine Barani Afrika.
Akizungumzia wajibu wa vyombo vya
habari katika kuzuia machafuko ambayo
yanaweza kupelekea kutoka kwa matukio ya uhalifu na makosa ya jinai
dhidi ya binadamu. Bi, Agnes kut Callamard kutoka Chuo Kikuu cha Columbia.
Amesisitiza haja na umuhimu kwa
waandishi wa habari kuzingatia maadili
ya kazi zao huku akitilia mkazo utendaji kazi huru wa vyombo hivyo ikiwa ni pamoja na haki ya kupata habari na kusambaza habari.
Amesisitiza kuwa uzoefu
umeonyesa kuwa sehemu nyingi
ambapo kumetokea machafuko, vyombo vya habari vimebainika kuchangia kwa asilimia kubwa uwepo wa hali
hiyo.
Naye B.i Peggy Hicks kutoka Human
Rights Watch akizungumzia kuhusu nafasi
ya asasi zisizo za kiserikali pamoja na mambo mengine amesema kuwa Tanzania ina mfumo mzuri unaoziwezesha asasi zisizo za kiserikali
kutekeleza majukumu yao pasipo kuingiliwa sana na serikali kuu. Na kusisitiza
asasi hizo za tanzania hazihitaji
kujifunza kutoka nje juu ya utekelezaji wa majukumu yao.
0 comments:
Post a Comment