Mwonekano wa mji wa Morogoro - Mjini. |
Kulingana na sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 315,866
Mji uko kando ya milima ya Uluguru. Ni kitovu cha viwanda vya mazao na mahali pa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro, Chuo Kikuu Kishirikishi cha Jordan, n.k.
Morogoro ni mji ujulikanao kwa muziki wa Kitanzania. Kwanza kabisa ilikuwa makao ya bendi maarufu ya Cuban marimba band chini ya mwanzilishi wake Salum Abdallah, mzaliwa wa mji huo. Makao makuu ya bendi hiyo yalikuwa Kichangani, mjini Morogoro. Nyimbo za santuri nyingi za miaka ya 1950 na 1960 zilitungwa mjini humo.
Mji huo ulikuwa makao ya bendi nyingine ya Moro jazz. Mwaka 1968, Mbaraka Mwinshehe, mwanamuziki mashuhuri wa Morogoro aliiwakilisha Tanzania kwenye maonyesho ya ulimwengu ya biashara yaliyokuwa mjini Osaka, Japan, na baada ya kurudi kwake alitunga wimbo uliokuwa maarufu nchini wa maonyesho hayo. Mbaraka alifariki kwa ajali ya gari mjini Mombasa, Kenya.
Mji wa Morogoro unajulikana kwa klabu za mchezo wa mpira. Wapenda mchezo huo watamkubuka mchezaji wa timu ya taifa Sembuli ambaye alikuwa mchezaji maarufu wa timu ya klabu ya Yanga.
Morogoro ni njiapanda ya barabara muhimu za Dar es Salaam - Mbeya na Dar es Salaam - Dodoma zinazokutana hapa.
Pana pia kituo cha reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, Mwanza na Kigoma. Reli ya TAZARA hupita nje ya mji mbali kidogo, katika kijiji cha Kisaki, wilaya ya Morogoro vijijini.
0 comments:
Post a Comment