Mgombea urais wa chama cha upinzani
cha FDC nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa na kuzuiliwa kwa muda na
maafisa wa polisi mjini Kampala.
Gari lake lilikuwa likipitia
barabara ya Jinja, mjini Kampala, msafara wake ukisindikizwa na mamia ya
wafuasi, pale polisi walipotumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi
hao na wakamkamata mwanasiasa huyo.![]() |
| Dkt Kizza Besigye amegombea urais dhidi ya Museveni mara tatu awali |
Alizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi cha Kira Road lakini akaachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka.
Polisi wanasema alikamatwa kwa sababu ya kutatiza uchukuzi mjini.
Mkuu wa Polisi Jenerali Uganda Kalekezi Kayihura amethibitisha kwamba polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani lakini akakanusha habari kwamba Bw Besigye amekamatwa.
Maafisa wengine wa polisi walisema kiongozi huyo wa upinzani alizuiliwa tu kwa muda.
Bw Besigye, alikuwa wakati mmoja daktari wa kibinafsi wa Bw Museveni, amekamatwa na kuzuiliwa mara nyingi lakini Jumatatu ilikuwa mara ya kwanza kukamatwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika Alhamisi.
Bw Besigye amewania urais mara tatu dhidi ya Bw Museveni bila mafanikio.
![]() |
| Wafuasi kadha wa Besigye wamekamatwa na polisi |


0 comments:
Post a Comment